Resources

Traisomi 21 (Down Syndrome) ni nini?

Ni hali ambayo inatokana na mtu kuwa na kromosomu ya ziada katika kromosomu ya 21. Kromosomu hii ya ziaida ndio inaleta changamoto ya ukuaji wa mwili wa mtoto wakati wa mimba na baada ya kuzaliwa. Hali hii sio ugonjwa kama inavyofikiriwa.

Kromosomu ni nini?

Kromosomu ni miundo inayofanana na uzi iliyoko katika kiini cha seli hai za wanyama na mimea. Kila kromosomu imetengenezwa na protini na molekuli  ya acid ya deoxyribonuclic acid (DNA). Kromosomu hurithishwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto zikiwa zimebeba maagizo/malezo maalamu(DNA) ambayo hufanya kila kiumbe kuwa cha kipekee.

Je ni kromosomu ngapi mtu huwa nazo?

Katika mwili wa binaadamu kila kiini cha seli hai huwa na seti ya kromosomu 23 ambayo inafanya jumla ya koromosomu 46. Seti 22 huwa zinafanana kwa wanawake na wanaume. Watu wanaoishi na hali ya traisomi 21 (Down syndrome) wanakua na chapa ya ziada katika seti ya 21, hivyo badili ya kuwa na chapa mbili wanakuwa na chapa 3 na kusababisha kuwa na jumla ya kromosomu 47. Chapa hii ya ziada husababisha mabadiliko na changamoto katika muenekano wa umbo na ukuaji wa akili wa mtu mwenye hali hii. 

Je watu wanaoishi na hali ya Traisomi 21 wana muonekano unaofanana?

Ni kweli watu wenye hali hii huwa wana muonekano unaofanana, ndio maana baadhi ya sehemu nchini Tanzania huwatambua kama watu wenye sura mfanano. Pamoja na kuwa na muonenako unaofanana kila mmoja ana uwezo wake wa kipekee na wakitofauti. Baadhi ya viashiria vinavyofanya wawe na muenakano sawa ni pamoja na, pua iliyo bapa, macho madogo yaliyo na muuondo wa duara dufu, mstari mmoja katika kiganja, shingo fupi, misuli dhaifu, huwa na kimo kifupi ukilinganisha na wenzao wa umri mmoja.

Je hali ya Traisomi 21 ni ya kurithi?

Aina zote za hali ya traisomi 21 zinatokana na maumbile (genetics) na kesi chache kiasi cha asilimia moja hutokana na kurithi.

Unaweza kufanya nini ili uweze kumtibu mtu mwenye hali ya Traisomi 21?

Hakuna matibabu kwa ajili ya kutibu hali ya Traisomi 21, kwasababu huu sio ugonjwa. Hata hivyo mtoto anaweza saidiwa katika maendeleo ya ukuaji wake kwa kumpatia matibabu ya msingi kuendana na mahitaji binafsi ya mwili na akili. Mtu mwenye hali ya Traisomi 21 anatakiwa kuona wataalamu tofauti wa afya wakiwemo, madaktari, wataalamu wa mazoezi tiba kwa vitendo, wataalamu wa mazoezi ya viungo, wataalamu wa tiba matamshi au mawasiliano na wataalamu wa saikolojia. Watu wenye hali ya traisomi 21 wakitegenezewa mazingira mazuri huweza kufikia hatua wanayostahili kufikia ingawa inaweza chukua muda zaidi ukilinganisha na watu wasio na hali hii. John Stephen Franklin ni muigizaji na mwanaharakati, Madeline Stuart ni mwana mitindo wa kimataifa na George Webster ni mtangazaji wa kimataifa ambao wote wanaishi na hali ya Traisomi 21.

Je ufanye nini ili usipate mtoto mwenye Traisomi 21?

Mpaka sasa hakuna namna yoyote inayojulikana inayoweza kumsaidia mtu asipate mtoto mwenye hali ya Traisomi 21. Hata hivyo wachunguzi wa kisayansi wametambua kwamba wazazi wote wawili wanaweza kumpa mtoto kromosomu ya ziada. Wazazi ambao teyari wana mtoto mwenye hali ya Traisomi 21 wana uwezekano wa asilimia 1 kupata mtoto mwingine mwenye hali hiyo. Kwa mwanamke mwenye umri mkubwa (Kuanzia miaka 35) ana uwezakano mkubwa wa kupata mtoto mwenye hali ya Traisomi 21.

Ni muda gani mtu mwenye hali ya Traisomi 21 huishi?

Mtu mwenye hali ya traisomi 21 huweza kuishi zaidi ya miaka sitini (60), kulingana na ukali wa shida za kiafya wanazoambatana nazo.

Ni shida gani nyingine za kiafya zinazohusiana na watu wanaoishi na hali ya Traisomi 21?

Baadhi ya watu wenye hali ya Traisomi 21 wanaweza kupata changamoto za kiafya, kama ugonjwa wa moyo, hatari ya kupata shida za kusaga chakula kama vile kuziba utumbo na kiungulia, kupata shida katika vichocheo vya mwili, pia shida za meno, nyama puani, matatizo ya kusikia na macho. Hivyo ni vyema kuongea na daktari wako ili kuchunguza, kutibu au kurekebisha magonjwa ambayo anaweza kuwa nayo kutona na kuwa na hali hii.

At Chadron’s Hope Foundation we are driven by a single goal: to improve the lives of people living with Down’s syndrome and developmental disabilities in Tanzania.

Contact

Opp. Wema Twins Tower, Basihaya TZ

Support

We are a small but mighty organization of volunteers so your donations can make a huge impact for those most vulnerable instead of covering overhead costs. Join us in this unique opportunity to directly change the lives of so many.

Copyright © 2014-2021 Chadrons Hope Foundation